Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Jedwali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jedwali la Wikipedia ni njia nzuri ya kupanga na kueleza data na namba, na wakati mwingine hata maelezo ya kimaandishi. Jedwali hupanga data, matini au picha kwa nguzo na misafa (=mistari).

Jedwali katika Wikipedia hutumia lugha ya misimbo isiyo vigumu sana lakini inadai matumizi ya makini kabisa. Wikipedia inaweza kuhaririwa pia kwa mfumo wa kihariri oneshi (VisualEditor), lakini maelezo yafuatayo yanahusu kihariri misimbo.

Ukurasa huu unakupa mifano kadhaa ya jedwali.

sehemu zinazoonekana hivyo zinanakiliwa na kumwagwa kwenye dirisha la hariri.
Maneno yaliyopo sasa ni mifano tu; badala yale weka namba na maandishi unayohitaji.

LAKINI usifute alama za misimbo kwa mfano "|", "|-" au "!".
ISIPOKUWA kwa njia inayoelezwa hapa kwa kuongeza au kupunguza misafa na nguzo.

Jedwali lenye nguzo 2 na misafa 2

Kichwa 1 (msafa 1) Kichwa 2 (msafa 1)
msafa 2, nguzo 1 msafa 2, nguzo 2
msafa 3, nguzo 1 msafa 3, nguzo 2

Jedwali hili la juu unalipata kwa njia ya misimo ifuatayo:

{| class="wikitable" border="1"
|-
!  Kichwa 1
!  Kichwa 2
|-
|  msafa 1, nguzo 1
|  msafa 1, nguzo 2
|-
|  msafa 2, nguzo 1
|  msafa 2, nguzo 2
|}

Nakili maandishi ya juu, bandika kwenye dirisha la hariri ya makala yako. Badala ya maneno kama "Kichwa 1" au "msafa 1, nguzo 2" andika namba au maandishi unayohitaji.

Jedwali lenye nguzo 3 na misafa 3

Kichwa 1 Kichwa 2 Kichwa 3
msafa 1, nguzo 1 msafa 1, nguzo 2 msafa 1, nguzo 3
msafa 2, nguzo 1 msafa 2, nguzo 2 msafa 2, nguzo 3

Jedwali hili la juu unalipata kwa njia ya misimo ifuatayo:

{| class="wikitable" border="1"
|-
!  Kichwa 1
!  Kichwa 2
!  Kichwa 3
|-
|  msafa 1, nguzo 1
|  msafa 1, nguzo 2
|  msafa 1, nguzo 3
|-
|  msafa 2, nguzo 1
|  msafa 2, nguzo 2
|  msafa 2, nguzo 3
|}

Nakili maandishi ya juu, mwaga kwenye dirisha la hariri ya makala yako na badilisha maneno kama "Kichwa 1" au "msafa 2, nguzo 3" na namba au maandishi unayohitaji.

Jedwali la kupanga

Ukitumia misimbo ifuatayo (wiki markup)

{| class="wikitable sortable"
|+ Jedwali la kupanga
|-
! scope="col" | Nguzo 1 (jina)
! scope="col" | Nguzo 2 (namba)
! scope="col" | Nguzo 3 (tarehe)
! scope="col" class="unsortable" | Nguzo isiyopangika (ukitaka)
|-
| jina a || 20 || 2008-11-24 || Nguzo
|-
| jina b || 8 || 2004-03-01 || hii
|-
| jina c || 6 || 1979-07-23 || haiwezi
|-
| jina d  || 4 || 1492-12-08 || ku-
|-
| jina e || 0 || 1601-08-13 || pangwa
|}

itaonekana hivyo:

Jedwali la kupanga
Nguzo 1 (jina) Nguzo 2 (namba) Nguzo 3 (tarehe) Nguzo isiyopangika (ukitaka)
jina a 20 2008-11-24 Nguzo
jina b 8 2004-03-01 hii
jina c 6 1979-07-23 haiwezi
jina d 4 1492-12-08 ku-
jina e 0 1601-08-13 pangwa

Kwa kubofya pembetatu ndogo unapanga jedwali lote upya.


Tazama pia

Bofya hapa ukitaka kubadilisha jedwali, kuongeza au kupunguza nguzo:

Wikipedia:Kubadilisha jedwali